Kipindi Mazungumuzo kwa amani : Huzurio ya wamama katika kuongoza nchi (Mwanabunge Katasohire, Mama Odile wa Huduma ya Jenda na Mwanasheriya Wasivinywa)

Kipindi Mazungumuzo kwa amani : Huzurio ya wamama katika kuongoza nchi (Mwanabunge Katasohire, Mama Odile wa Huduma ya Jenda na Mwanasheriya Wasivinywa)

12. juin 2024 Allgemein 0
Partager les articles de Radio Elimu UOR

Msikilizaji mpenzi, jambo.

Tunakukaribisha katika kipindi hiki MAZUNGUMUZO KWA AMANI, utayarishaji Muungano wa Shirika za Wamama, CAF ASBL kwa kushirikiana na Search For Common Ground. 

Leo, tuta zungumuziya kiwango ambacho tayari kimefikiwa katika kuhuzuria kwake mama katika uongozi wa  nchi ya Congo, iwe kwa kutajwa ao iwe kuhusu ku chaguliwa .

Kama unavyojua, kuna Waziri Mkuu ambaye anaongoza Serikali ambaye atatimiza programu yake Rais tshisekedi.

Serikali yake ina zaidi ya asilimia 30 ya uwakilishi wa wanawake.

Katika ngazi ya kuchaguliwa, Butembo ina mwanabunge wa kwanza wa taifa, mama aliyechaguliwa.

Huyu ni Kavira Katasohire Jeanine ambaye pia alichaguliwa katika eneo la Beni kama mwanabunge wajimbo. Katika kipindi hiki, mteule huyu atatuambia kuhusu furaha yake na changamoto zinazomngoja. Naye Léonie Mulyangote, ambayeni mwanabunge kijimbo, pia ata tuambia mawili kuhusu kazi yake.

Kwa upande wake, Huduma ya Jinsia, Familia na Watoto pa Butembo ina shangiliya kiwango ambacho kime  fikiwa katika huzuriyo ya mama katika uongozi wa nchi.

Kwa hivyo, Chef de Bureau Odile Mabanza Dibi ana sema kuna hatua mupya katika utekelezaji wa Azimio 1325 inayo wekeya mkazo usawa kati ya wanaume na wanawake.

Katika kipindi hicho tena, REDHO ina shukuru pia uwakilishi wa wanawake ambao huongezeka kutoka 17 hadi zaidi ya asilimia 30. Mratibu wake, Mwanasheriya Muhindo Wasivinywa, anaenda mbali na kuomba hata jimbo  za Kivu Kaskazini na Ituri ziongozwe na wamama ili ya kurudisha usalama ambao wababa hawaja weza  bado kuketisha.

Anaye ku leteya kipindi hicho ni  Patient Akilimali

Sikiliza  uki funyanga PLAY